Jumatatu , 20th Sep , 2021

Shirikisho la soka duniani (FIFA) Limealika mashirikisho ya soka yaliyopo chini yake, siku ya septemba 30, 2021 kujadili juu kalenda ya kimataifa ya mpira wa miguu na pendekezo la Mkuu wa Maendeleo ya Soka Ulimwenguni , Arsene Wenger kuandaa Kombe la dunia kila baada ya miaka miwili.

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino akizungumza kwenye moja ya mkutano wa shirikisho hilo mwaka huu.

Ikiwa hivyo, Shirikisho la mpira nchini Tanzania (TFF) kama mshirika wa FIFA, itapata nafasi ya kushiriki katika mkutano huo unaokumbana na pingamizi kutoka UEFA chini ya Rais Aleksander Ceferin kuhusu wazo la kuwa na kombe la dunia kila baada ya miaka miwili.

"Hii ni moja wapo ya fursa kadhaa za kuanzisha mijadala ya wazi kujenga, katika kiwango cha kimataifa na kikanda, katika miezi ijayo na FIFA inatarajia kufanya hivyo.”

“Kwakuwa huu ni mradi wa mpira wa miguu, yanalenga masilahi ya ulimwengu na mpira wa miguu yanapaswa kutangulizwa, mchakato huu ambao ulianza na wachezaji na makocha kutoka kote ulimwenguni.” Ilisomeka kauli ya FIFA iliyotoka siku ya leo.