Jumatatu , 10th Jan , 2022

Mahakama ya Australia imeamuuru kuwa mchezaji namba moja kwa ubora Duniani kwenye Tenisi,Novak Djokovic kuachiliwa huru na kwenda kushiriki michuano ya wazi ya Australia licha ya kuwa hajapata chanjo ya UVIKO-19.

Hakimu wa kesi hiyo amesema kuwa ameona kuwa hakuna madai yoyote ya msingi kufuatia kuzuiliwa kwa hati ya kusafiria ya Djovo na Ofisa wa mpakani katika uwanja wa ndege wa Melbourne.

Jaji Antony Kelly ameamua hati ya kusafiria aliyokuwa anatumia Djokovic ni halali na anaruhusiwa kuingia nchini Australia ilikuweza kuweza kushiriki mashindano ya wazi ya Australia.

Mashindano ya Australia Open yanatarajia kuanza Januari 17, ambapo Djokovic ndiye, anaingia kwenye michuano hiyo kama bingwa mtetezi akiwa ameshinda taji hilo mara tisa.