Dickson Job ni Mwananchi, asaini miaka 2 na nusu

Jumatatu , 11th Jan , 2021

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kati wa kimataifa wa Tanznaia Dickson Job kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mkataba wa miaka 2 na nusu, mchezaji huyo ametangazwa rasmi hii leo.

Dikson Job kulia akiwa na makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga ENG. Hersi Saidi

Dickson Job anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu ya Yanga katika dirisha hili dogo la usajili baada ya klabu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji mrundi Saidi Ntibazonkiza. Job amesaini mkataba wa miaka 2 na nusu wa kuitumikia timu ya wananchi.

Baada ya usajili huu sasa klabu ya Yanga inakuwa na idadi ya mabeki wa kati wa 5, ambapo safu hiyo inaongozwa na nahodha Lamine Moro, Bakari Nondo Mwamnyeto, Abdalla Haji Shaibu maarufu Ninja na Saidi Juma Makapu.

Dickson mwenye umri wa miaka 20 kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanznaia Taifa stars ambayo ipo kwenye maandalizi ya kujiandaa na michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ligi za ndani, itakayoanza kutimua vumbi Januari 16, 2021 nchini Cameroon.