Jumatano , 28th Sep , 2022

Mshambuliaji wa Simba Mserbia Dejan Georgijević ametangaza kuachana na klabu hiyo kwa kile alichokiandika kwamba Simba wameshindwa kutimiza baadhi ya matakwa yaliyopo kwenye mkataba wake.

Dejan Georgijevic

Kupitia ukurasa wake binafsi wa Instagram,Dejan ameandika Nathibitisha rasmi  kuwa mkataba wangu wa Ajira umevunjika kutokana na baadhi ya vipengele kukiukwa na Klabu ya Simba. Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga Mkono na kunionesha Upendo.

Nyota Dejan Georgijević alijiunga na klabu ya Simba mnamo Agosti 7 - 2022 akitokea klabu ya NK Domzale ya nchini Slovenia huku usajiri wake ukitajwa kuwa ulikuwa ni matakwa ya aliyekuwa kocha mkuu wa Simba Zoran Maki na ameitumikia Simba michezo 9 na kufunga bao 1 pekee kwenye michezo yote aliyoitumikia kwa msimu huu.

Dejan  anaondoka kwenye kikosi hicho akiwa amefunga bao moja tu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar Agosti 20, wakati Simba iliposhinda mabao 2-0, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.