Jumatatu , 5th Apr , 2021

Beki wa kati wa Juventus Matthijs De Ligt amesema anajuta kusaini Juventus na kuacha timu nyingine mbalimbali kubwa zilizo muhitaji zikiwemo Manchester United na Barcelona.

Beki De Ligt wa Juventus akiwa ameshika kichwa aamini kinachoendelea katika moja ya mechi ya Serie A

De ligt beki wa kati kutoka Uholanzi ambaye alikuwa kwenye kiwango cha juu sana katika msimu wa mwaka 2018/2019 akiwa na Ajax Amsterdam ambapo walifanikiwa kucheza nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya wakatolewa na Tottenham kwa bao 3-2.

Ajax ilikuwa na wachezaji vijana wazawa wa uholanzi waliokuwa katika kiwango bora sana akiwemo Frankie de Jong aliyejiunga na Barcelona, Dony van de Beek ambaye baadaye alitimukia Manchester United.

Kizazi chao hiki ambacho kimetawanyika katika ligi tatu tofauti miongoni mwa 5 bora Ulaya, EPL La liga na Serie A bado hakijapata mafanikio makubwa kama watu walivyotarajia,hali inayomfanya ajute wepo wake ndani ya Juventus.

De Ligt amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Serie A akiwa na Juventus katika msimu wa 2019/2020 lakini kwa sasa hana furaha na maisha ya Turin, huku hamu ya kujiunga na Barcelona ikiwa kubwa kwa sababu ya uwepo wa kocha Ronald Koeman.

Mwenendo wa Juventus kwa sasa si mzuri wapo katika nafasi ya 4 wakiwa na alama 56 katika michezo 28 walioshuka dimbani, huku ligi ikiongozwa na Inter Milan yenye alama 68 wakiwa nyuma kwa alama 12 na michezo iliyobaki ni 10 tu.