Ijumaa , 7th Jan , 2022

Nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry na Kevin Durant wa Brooklyn Nets ndiyo wacheza kikapu wanaoongoza kwa kupigiwa kura nyingi na mashabiki ili waingie kwenye kikosi cha NBA All Stars kwa msimu huu 2021-22.

Steph Curry (Kushoto) akimzuia Kevin Durant kwenye moja wapo ya michezo ya NBA.

Curry anaongoza akiwa amepigiwa kura milioni mbili laki tano na themanini na nne, Durant wapili akiwa na kura milioni mbili laki tatu na siti, MVP wa fainali za NBA msimu uliopita Giannis Antetokounmpo watatu na Lebron James wanne.

Mchakato wa upigaji kura unaendelea na matokeo mengine ya kura hizo yatawekwa wazi Januari 20 mwaka huu na wachezaji hao wataunda timu mbili kutoka ukanda wa Mashariki na Magharibi na kucheza mchezo Februari 20,2022.