Cheka atwaa ubingwa wa UBO

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Bondia wa Tanzania, Cosmas Cheka ameshinda pambano dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

Bondia Cosmas Cheka akikabidhiwa ubingwa wa UBO baada ya ushindi dhi ya Hannock Phiri.

Mabondia hao walipigana wa uzito wa Light kuwania UBO International Title ambapo pambano hilo lilikuwa la round 12.

Kwa uamuzi wa majaji ameonekana kushinda japo mpinzani wake ameonekana kutokubaliana na uamuzi huo wa kupoteza pigano hilo.

Mbali na hayo, Cheka amesema kuwa kama mpinzani wake hajaridhika, arudie pambano na kwamba yeye yuko tayari kumfuata Malawi.

Katika Mapambano ya utangulizi, Mwanadada Zulfa Macho, mtoto wa Yusuph Macho alishinda kwa Knock-Out kwenye round ya kwanza kwenye pambano dhidi ya Mmalawi, Ndau Chilimba