Jumamosi , 26th Sep , 2020

Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa Ushirika uliopo Moshi mkoani Kilimanjaro kuchezewa mechi zozote za mashindano.

Uwanja wa Ushirika Moshi ni uwanja wa tatu kufungiwa na Bodi ya Ligi msimu huu

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya ligi imeelza uwanja huo umefungiwa kutokana na kukosa baadhi ya sifa za kikanunu kama zilivyoainishwa kwenye Kanuni ya Saba inayozungumzia uwanja na sheria namba moja ya mpira wa miguu inayozungumzia uwanja.

kutokana na uamuzi huo wa kuufungia uwanja wa Ushirika, Bodi ya Ligi imeitaka klabu ya Polisi Tanzania kuutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini Arusha kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za Ligi kuu ya Vodacom 2020-21.

lakini pia Kamati ya Leseni za klabu itaufanyia uchunguzi uwanja huo baada ya marekebisho kukamilika.

Huu unakuwa ni uwanja wa tatu kufungiwa na Bodi ya Ligi msimu huu kwa kukosa sifa za kikanuni, viwanja vingine vilivyofungiwa ni uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani ambao ni uwanja wa nyumbani wa Ruvu Shooting na uwanja mwingine ni wa Gwambini Uliopo Misungwi Jijini Mwanza ambao ni uwanja wa nyumbani wa Gwambina FC.