Jumatatu , 12th Feb , 2024

Bingwa wa michuano ya Afcon 2023 Ivory Coast amejinyakulia kitita cha dola milioni 7(7,000,000) ambayo ni zaidi ya Bilioni 17.7 kwa fedha za Kitanzania baada ya kuifunga Nigeria magoli 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Februari 11-2024 mjini Abdijan nchini Ivory Coast.

Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na nyota Frank Kessie na Sebastian Haller huku bao la Nigeria likifungwa na mlinzi Troost Ekong huku Super Eagles ambao ni washindi wa pili wameondoka na Dola Milioni 4 (4,000,000) zaidi ya Bilioni 10.1 kwa  fedha  za Kitanzania

Upande mwingine, Golikipa Ronwen Williams wa Afrika Kusini  ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano,Emilio Nsue Lopez ameshinda tuzo ya mfungaji bora baada ya kuifungia Equatorial Guinea mabao5 ilhali nahodha wa Nigeria William Troost-Ekong akichaguliwa kuwa mchezaji bora mashindano ya Afcon 2023.