Wafungaji wa mabao ya Azam dhidi ya KMKM Ayub Lyanga na Akuno Akuno wakishangilia moja ya goli waliofunga
Magoli ya Azam jioni hii yamefungwa na mshambulia Ayub Lyanga kunako dakika ya 18 lile la pili lilifungwa na mshambuliaji toka Cameroon Akono Akono dk 90, ambaye bado hajaanza kuonekana katika kikosi cha Azam katika michezo ya ligi kuu,
Azam kwa sasa wanajivunia mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube, ambaye alikosekana katika kikosi cha leo kutokana na kuwepo katika majukumu ya Taifa lake ,ambapo walikuwa na mchezo dhidi Algeria ulimalizika kwa sare 2-2 huku naye akifunga goli
Wadau wengi walitaraji Azam isingepata ushindani mkubwa kutokana na kumkosa mfungaji wao bora kwa sasa Prince Dube mwenye magoli 6 katika ligi kuu ya VPL inayoendelea , hata hivyo walifanikiwa kuibuka na ushindi huo, KMKM toka Zanzibar wamekuwepo Tanzania bara kwa kwa michezo kadha ya kirafiki