Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa taarifa hiyo na kusema mechi hiyo imehamishiwa Chamazi ilikupisha shughuli hizo
"Tumepata taarifa kutoka serikalini asubuhi kuwa Uwanja wa Taifa kesho unatumika kwa shughuli za kitaifa hivyo hatutaweza kucheza mechi yetu hapo na kama unavyojua hatuwezi kubishana na Serikali. Tunaishukuru Azam kwa kutukubalia mechi yetu tuihamishie kwenye uwanja wao, hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi Chamazi kushuhudia mchezo huo kama walivyofanya katika mchezowa awali ambapo viingilio vitakuwa Sh7,000 kwa VIP na Sh 5,000 mzunguko." alisema Mkwasa.
Mkwasa alisema baada ya mchezo huo wa kesho, Yanga itaondoka Jumapili asubuhi kwenda Zanzibar na usiku itacheza mechi nyingine ya kirafiki na Mlandege itakayofanyika kwenye Uwanja wa Aman na baadaye kuelekea Pemba kujifua kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayofanyika Agosti 23.