Atalanta Hawks yamtimua Lyoyd Pierce

Jumanne , 2nd Mar , 2021

Timu ya Atalanata Hawks inayoshhiriki ligi ya kikapu nchini Marekani NBA, imethibitisha kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wake, Lyoyd Pierce sababu ikielezwa, timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo pamoja na hali ya kutoelewana kwa baadhi ya wachezaji nyota.

Kocha wa Atalanta Hawks, Lyoyd Pierce aliyetimuliwa kazi.

Lyoyd ambaye ameiongoza Atalanta Hawks kwa muda wa misimu miwili na nusu, ameiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya 11, wakishinda michezo 14 na kupoteza michezo 20 katika michezo 34 waliyocheza mpaka hivi sasa kwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa ugomvi uliopo kati ya nyota wawili wa timu hiyo,Traae Young na John Collins umepelekea kocha huyo kufukuzwa kutokan ana kushindwa kuusuluhisha na hatimaye kuleta mpasuko miongoni mwa wachezaji kwenye kambi ya timu hiyo na kupelekea matokeo mabaya.

Kwa upande mwingine, Atalanta Hawks inataraji kushuka dimbani alfajiri ya kuamkia kesho kucheza dhidi ya makamu bingwa wa ligi hiyo, Miami Heat ilhali bingwa mtetezi wa ligi hiyo, timu ya LA Lakers watacheza na Phoenix Suns.