
Andy Murray akijaribu kuukosa mpira kwenye mashindano ya Moselle Open nchin Ufaransa.
Baada ya Andy Murray kutinga hatua hiyo, sasa anasubiri kucheza na mshindi wa mchezo wa mtoano wa 16 bora utakaowakutanisha Mfaransa Lucas Pouille na Hurkacz Hubert wa Poland usiku wa leo nchini humo.
Murray ambaye alicheza fainali ya Moselle Open mwaka 2007 amesema anachukulia mashindano hayo kama daraja la kurudisha ubora wake uliopungua makali mara baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili na kumfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu na kuporomoka kwenye viwango vya ubora nchini England na Duniani.