Alichosema Neymar baada ya kutolewa kadi nyekundu

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Neymar Jr alikua miongoni mwa wachezaji watano waliotolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa ambao PSG ilifungwa kwa bao 1-0.

Neymar Jr na Alvaro Gonzalez wakijibizana katika mchezo uliopigwa suki wa kuamkia leo.

Wakati anaondoka uwanjani Neymar alimwambia mwamuzi wa akiba kuwa alisikia maneno ya kibaguzi kutoka kwa mchezaji wa Marseille.

Leandro Paredes na Layvin Kurzawa kwa upande wa PSG na Jordan Amavi na Dario Benedetto wa Marseille walijumuishwa kwa pamoja walionyeshwa kadi nyekundu.

Kabla ya kadi hiyo nyekundu,mwamuzi alikwenda kutazama video ya usaidizi (VAR) na kubainia Neymar alimpiga nyota wa Marseille Alvaro Gonzalez.

Ugomvi ulitokana na nyota wa Marseille , Benedictto kumsukuma Paredes wa PSG ambaye pia alirudishia na kuleta taharuki.

Katika tukio hilo wachezaji Lavyin Kurzawa wa PSG na Amavi walionyeshana ubabe kiasi cha kuonyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja.