Jumanne , 13th Feb , 2024

Nyota kutoka nchini Congo anayekipiga katika klabu ya Rayon Sport ya nchini Rwanda, Héritier Luvumbu, amevunjiwa mkataba na klabu yake kisa kuonesha ishara ya uzalendo kwa nchi yake.

Héritier Luvumbu mara baada ya kufunga goli alishangilia kwa Ishara ya kuweka mkono juu ya mdomo na vidole kichwani staili ambayo inaashiria kupinga mauaji yanayoendelea nchini Congo.

Ishara hii pia imewahi kutumiwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Congo wakati wakiimba wimbo wa taifa kwenye mchezo wa nusu fainali ya AFCON dhidi ya Ivory Coast.