Jumatatu , 6th Dec , 2021

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka barani Afrika, Abdel Moniem Shatta ametilia shaka maandalizi ya AFCON yanayotazamiwa kufanyika mapema 2022 kwasababu wenyeji Cameroon kusua sua kukamilisha ujenzi wa viwanja.

(Kombe la Michuano ya Mataifa ya Afrika 'AFCON' 2022)

Wasiwasi huo unaibuka baada ya kamati ya mashindano hayo kufanya ukaguzi nchini Cameroon kuona kuwa, muda uliosalia huenda usitoshe kukamilisha ujenzi wa viwanja hivyo hususani eneo la kuchezea.

Ripoti ya tathmini kutoka kamati hiyo imeeleza kuwa, hata ikitokea michuano hiyo ikisogezwa mbele kwa muda wa miezi 3au 4 basi hakuna nchi ambayo itaweza kukamilisha maandalizi hayo hivyo huenda yakafutwa kwa mwaka 2022.

Shirikisho la soka la kimataifa Ulimwenguni FIFA linaelezwa kufuatilia maandalizi hayo kwa ukaribu huku ikiripotiwa kuwa tayari kuridhia michuano hiyo ifanyike nje ya bara la Afrika licha ya kuhusisha mataifa 24 na si 16 tena.

Mdokezo wa michuano hiyo kuhusishwa kufanyika hata nje ya bara la Afrika umekuja baada ya uwepo wa Katibu Mkuu wa FIFA, Bi. Fatma Samoura (Senegal) nchini Cameroon.