Yusuph Mlela ajibu kuhusu kujiweka mwanamke

Jumatatu , 20th Jul , 2020

Msanii wa filamu Yusuph Mlela amefunguka kuhusu lifestyle yake na kusema, atafanya vitu vyote kama kusuka au kuvaa hereni lakini hawezi kujiweka kama mwanamke japo wapo wengine wanaofanya hivyo.

Msanii wa filamu Yusuph Mlela

Yusuph Mlela ambaye aliwahi kushiriki uwanamitindo amesema kwa kuwa yeye ni msanii, anatakiwa kubadilika kimuonekano ili kupendeza na kuonekana fresh ila hawezi kujifanya kama mwanamke.

"Style yangu ya kusuka napendeza na kuonekana fresh kwa sababu mimi ni msanii natakiwa nibadilike badilike, kama leo ukiniona nina para kesho unikute na nywele, kitu ambacho siwezi kufanya kwenye hii lifestyle ni kujiweka kama mwanamke, kila mtu yupo na anavyojihisi lakini kama mimi Mlela siwezi kufanya hivyo" ameeleza Yusuph Mlela.

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.