Jumatano , 13th Mei , 2020

Msanii wa HipHop hapa nchini Tanzania Young Killer, amenyoosha maelezo juu ya madai ya kutomsaidia Baba yake pia amefunguka kuhusu kupata mtoto wa kike mwishoni mwa mwaka 2019.

Msanii wa HipHop Young Killer

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, wakati anajibu tuhuma za kutomsaidia mzazi wake huyo wa kiume Young Killer amesema,

"Baba yangu hawezi kuja kwenye vyombo vya habari na kuongea vitu kama hivyo, huyo hawezi kuwa mzee wangu, mimi natoa mahitaji kwa familia yangu sio kwa mzee tu yaani ukiwajumlisha wote kuanzia Baba, Mama na Dada, huyo mzee aliyesema hivyo itabidi amtafute mwanaye sio mimi" ameeleza Young Killer.

Aidha akizungumzia kupata mtoto na mipango ya kuingia kwenye ndoa msanii huyo amesema  "Nimepata mtoto wa kike na nilikuwa nataka mtoto mwenye jinsia hiyo, namshukuru Mungu nimefanikiwa, tutegemee chochote kwa sababu Mungu ndiyo mpangaji wa kila kitu na chochote kitakachotokea tutaishi nacho maana hatuifahamu kesho yetu lolote linaweza kutokea".

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini