Jumatatu , 15th Apr , 2024

Rapa Young Killer Msodokii mama yake mzazi na mpenzi wake wametembelea Gereza Kuu Butimba Mwanza kutoa misaada ya Dawa za meno, Miswaki, Mafuta na Juice kwa wafungwa wa gereza hilo.

Picha ya Young Killer na Mkuu wa Gereza la Butimba Mwanza

“Nimefurahi sana leo kufika Gereza Kuu Butimba Mwanza, kukutana na ndugu zetu waliopata chagamoto za kuwapelekea kuwa gerezani. Ninamshukuru sana mwenyezi MUNGU kunipa hii nafasi ya kuwatembelea ndugu zetu” - ameandika Young Killer

Kupitia Video hii inaonesha Young Killer alivyopokelewa na Mkuu wa Gereza hilo na kumuunga mkono kitendo alichofanya.