Jumanne , 10th Oct , 2023

Kila ifikapo tarehe 10/10 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Afya ya akili ulimwenguni, kwenye kuadhimisha siku hii mtandao wenye watumiaji zaidi ya Bilioni 2.7 kwa mwezi ''WhatsApp'' umeamua kuadhimisha kwa namna ya tofauti siku hii.

 

Namna ambavyo WhatsApp wameamua kuadhimisha siku hii, Ni kwa kuonesha namna ambavyo mtumiaji wake anaweza kuhakikisha anakuwa sawa na kuimarisha afya yake ya akili kwa kuepukana na vitu vichache vinavyoweza kupelekea mfarakano na mvurugano wake wa akili.

Hivi ni vitu baadhi ambavyo WhatsApp wameonesha ikiwa kama sehemu ya kuadhimisha siku hii

1. Chat lock (Kuficha mazungumzo yako)
2. Silence unknown callers ( kuzuia namba ngeni kukupigia kwa njia ya WhatsApp)
3. Disappearing Messages and View once (Ujumbe kutokewa baada ya kupokelewa)

Namna zinavofanya kazi,
Chat lock (Kuficha mazungumzo)
1. Fungua WhatsApp yako.
2. Fungua mazungumzo unayotaka kuficha (chats).
3. Gusa sehemu ya juu kwenye picha itakupeleka kwenye ''profile''.
4. Shuka chini mpaka kwenye chaguo la ''Chat Lock'' 
5. Iwashe na utachagua namna ya kuficha iwe ni ''Fingerprint au Password".
6. Thibitisha uwekaji wa ''Fingerprint au Password".

2. Silence unknown callers ( kuzuia namba ngeni kukupigia kwa njia ya WhatsApp)
1. Kwenye WhatsApp yako ingia ''Setting kisha Privacy''
2. Gusa palipoandikwa ''Calls''
3. Utaona palipoandikwa ''Silence uknown calls'' 
4. Isogeze kwa kuelekea upande wa kulia kuruhusu/kuiwasha

3. Disappearing Messages and View once (Ujumbe kutokewa baada ya kupokelewa)
1. Fungua kwenye mazungumzo husika kwenye mtandao wa WhatsApp
2. Gusa upande wa juu ambapo jina la muhusika linasomeka
3. Shuka chini chagua palipoandikwa ''Disappearing Messages''
4. Bonyeza endelea (Continue) kisha ruhusu kukubali (Turn it on)

Kwenye kulinda faragha za mtumiaji wa mtandao wa WhatsApp, WhatsApp wameonesha namna ambavyo wanaweza kulinda afya ya mtumiaji wake. Huenda ukawa shuhuda wa baadhi ya watu walioingia kwenye msongo wa mawazo baada ya faragha zao kuvuja na kusambaa mtandaoni.
Picha: WhatsApp