Alhamisi , 5th Oct , 2023

WhatsApp wameanza kufanya majaribio ambayo yatamuwezesha mtumiaji wake, ku-pin ujumbe sehemu ya juu kwenye ''chats'' ndani ya group kama ilivyokuwa inafanyika kwenye ''chats'' za kawaida.

 

Kwa kushikilia ujumbe, itakuwezesha kupata chaguo jipya la ''Pinned Message'' bila kujali iwapo kuna jumbe nyingine zimetumwa kwa wakati huo, Na pia kutakuwako na muda wa kuweka ujumbe huo, na machaguo hayo yatakuwako ni kwa muda wa saa 24, siku 7 au kwa muda wa siku 30 na vile vile utaweza kuondoa ujumbe huo kwa muda wowote utakao ''Unpinned"

Kwa sasa watumiaji wa ''WhatsApp beta'' ndiyo ambao wanawezeshwa kupata chaguo hili, hivyo bado haijafahamika ni nani haswa ambaye ataruhusiwa ku-pinned message kwenye group husika, ikiwa kama ni kiongozi (admin) au mtu yeyote.