Alhamisi , 19th Oct , 2023

Mtandao wa ''X'' ambao awali ulikuwa ukifahamika kama Twitter, umetangaza kuanza kutoza kiasi cha Dola moja (1) kwa mwaka ambayo ni sawa na kiasi cha shilingi 2,500

kwa watumiaji wapya ili kuweza kutumia mtandao huo haswa kwenye vitu muhimu kama vile ku-tweet, ku-reply, ku-quote, ku-repost, ku-like, bila kusahau wazee wa bookmark.

Kampuni ya hiyo inaamini kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondoa uwepo wa akaunti feki (maroboti) kwenye mtandao huo.

Na mfumo huu utaanza kama majaribio kwenye baadhi ya nchi.

Picha: Business Today