Picha ya familia ya Marino Vaneenoo na Gwenny Blanckaert
ambapo familia hiyo yenye jumla ya watoto 11 ( wa kike 7 na wa kiume 4) imekuwa ikitumia herufi 4 zinazofanana katika kuwapa majina watoto wao wote 11, na herufi hizo ni (A , X ,E na L).
Mtoto wa kwanza katika familia hiyo ni Alex ana miaka 13, akifuatiwa na Axel,( 12), Xela, (11), Lexa,( 10), Xael, (9), Xeal, (8),Exla, (5), Leax,( 4), Xale, (2), Elax,(1), na Alxe ambaye ana miezi 6.
Hivi karibuni wazazi hao wanatarajia kupata mtoto wao wa mwisho wa kiume mwezi Aprili mwaka 2022 ambaye atakamilisha idadi ya wototo 12.