Jumanne , 10th Oct , 2023

Zamani ukifahamika kama Twitter lakini ''X'' kwa sasa, Mtandao huu umepanga kuja na chaguo jipya kwa watumiaji wake ambao wamelipia huduma ya ''Verification check-mark''

Chaguo hili litamuwezesha mtumiaji wake kuchagua watu ambao watawezeshwa kujibu (Reply)  kwenye chapisho (post) ambayo muhusika atakuwa ameweka kwenye mtandao huo.

Ilivyo ni kama ile ambayo baadhi ya watu wanaitumia kwenye mtandao huo, pale ambapo anahitaji kundi fulani la watu ndiyo waweze kujibu kwenye chapisho husika.

Lakini utofauti wake ni kwamba hii mpya mtumiaji ataruhusu wenye vitiki pekee kujibu kwenye chapisho husika