Jumatano , 18th Oct , 2023

Kwa mujibu wa wavuti wa CDC unaandika, kila uchwao watu zaidi ya 3,700 wanapoteza maisha na chanzo ikiwa ni ajali za barabarani. Na nusu kati ya hao ambao hufariki kwa ajali za barabarani ni watembea kwa miguu na waendesha pikipiki.

 

Kwa mujibu wa wavuti wa Forbes.com unaandika kuna sababu kuu mbili zinazopelekea ajali za barabarani moja ikiwa ni mwendokasi wa dereva na mbili ikiwa ni ulevi wa madereva.

Mpaka kufikia mwaka 2022 utafiti kutoka shirika la afya ulimwenguni ''WHO'' ulikuwa na idadi ya watu 630, 000 wanaofariki kwa HIV/AIDS kwa mwaka. huku jarida la CDC likitaja watu zaidi ya Milioni 1.35 ambao hufariki kwa ajali za barabarani kwa mwaka (Jan, 2023).

Dunia kwa sasa imekuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na Ajali za Barabarani, huku  kwa asilimia kubwa sababu ikiwa ni uzembe wa dereva. 

Teknolojia inaweza kuwa mkombozi kwenye kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za barabarani haswa kwa watumiaji wa kawaida (watembea kwa miguu).

Hizi ni baadhi ya teknolojia ambazo tunaweza kuzitumia ili kupunguza ajali za barabarani, 

Pedestrian Detection Systems: Kwenye magari ambayo ni matoleo ya hivi karibuni yako kwenye sehemu nzuri ya kuwa na vitambuzi au kamera ambazo zinauwezo wakubaini iwapo mbele au nyuma ya gari kuna mtu au pikipiki.

Automatic Emergency Braking: Hii ni teknolojia ambayo inawekwa ndani ya gari na hufanya kazi pale ambapo imetokea dharura na breki ya gari inatakiwa iwe haraka kufanya kazi, mfano iwapo Dereva ilikuwa agongane na gari, pikipiki au mtu.

Vehicle-to-Infrastructure (V2I) Communication: Hii ni teknolojia ambayo mtuamiaji wa barabara (mtembea kwa miguu) kupitia simu janja anawezeshwa kuarifu taa za barabarani iwapo atahitaji kuvuka barabara kwa muda huo.

Hizo ni baadhi tu ya teknolojia ambazo tunaweza kuzitumia kwenye kupunguza ajali za barabarani, kwa upande wako mwana-tech unahisi ni ipi ambayo inaweza kuwa nzuri kwenye ukanda huu wa Afrika mashariki?

Picha: AP News