Vitu 5 vya kuzingatia ukishanunua simu mpya

Jumanne , 1st Dec , 2020

Ukishanunua simu mpya, kila mmoja anakuwa na haraka ya kufungua boksi kuiwasha simu yake na kuanza kutumia, sasa hivi ni vitu 5 muhimu vya kuzingatia baada ya kununua simu mpya ( kwa leo tutaziangazia simu za Andoid )

Vitu 5 vya kuzingatia ukishanunua simu mpya

Angalia 'updates' mpya za Apps kwenye simu yako

Ukishaiwasha nenda kwenye mpangilio wa simu (settings), kisha nenda kwenye kuhusu simu (About device), kisha Software updates. Kufanya hivi inasaidia kuifanya simu kufanyakazi kwa ufanisi, kuimarisha ulinzi na kuongeza uimara.

Ondoa Apps ambazo huzihitaji

Hatua nyingine muhimu ni ya kuondoa Apps ambazo hazina umuhimu zinazokuja moja kwa moja kwenye simu ili kuongeza nafasi ya simu yako.

Nakili data zako kutoka kwenye simu ya awali

Ukiwa unaseti vitu vyako kwenye simu mpya, Androids itakuuliza wapi unataka kunakili (copy) taarifa zako kutoka kwenye kifaa cha zamani, ambapo unaweza kutumia USB cable inayoendana au kwa kutumia Apps za kuhamishia taarifa mbalimbali.

Angalia Apps za chaguo msingi (Default Apps)

Ziangalie 'Default Apps' kwenye simu yako na uzipangilie kwa namna unayotaka. Ili kuzipata ingia kwenye Mpangilio wa simu (settings), kisha Apps & Notifications, kisha Default Apps.

Wezesha kipengele cha kuitafuta simu yako ( Find my Device )

Huduma ya kutafuta simu yako kutoka Google itakuwezesha kuitafuta, kuifunga na kuizima kabisa pindi inapopotea, kwahiyo hakikisha unaiwezesha simu yako na huduma hii tangu siku ya kwanza.

Ili kuwezesha simu yako, nenda kwenye mpangilio wa simu (Settings), kisha ulinzi (Security), kisha tafuta kifaa changu (Find my Device) na kuwasha. Hakikisha ukiwa unafanya hivyo, umewasha data na 'location'.