Jumatatu , 25th Oct , 2021

Viatu vya Air Jordan vilivyokuwa vikitumiwa na nyota wa zamani wa mpira wa kikapu wa Chicago Bulls, Michael Jordan vimevunja rekodi ya mnada kwa kuuzwa bei kubwa  zaidi ambayo ni dola Milioni 1.47 zaidi ya Ths. Bilioni 3.

Picha ya Michael Jordan, nyota wa zamani wa mpira wa kikapu wa Marekani

Bei hiyo ndio ya juu zaidi kwa viatu vya michezo, na Jordan alitumia viatu hivyo aina ya Nike Air Ships vyenye rangi nyekundu na nyeupe wakati wa msimu wake wa kwanza akiichezea timu ya Chicago Bulls.

Huo ndio mwaka yeye na Nike walianza ushirikiano wao kuunda nguo zenye nembo yake na viatu. 

Jordan anaaminika na wengi kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa vikapu.Jordan ambaye kipindi kirefu aliichezea timu ya Chicago Bulls alikuwa nyota na kuweza kuinua kiwango cha mchezo huo kote duniani.

Jordan ambaye alistaafu mwaka 2003 alikuwa mchezaji wa kwanza bilionea katika historia ya NBA .