Jumatatu , 11th Oct , 2021

Huwenda hii ikawa ni habari njema kwa watumiaji wa mtandao wa kijamii wa TikTok, baada ya Oktoba 8 mwaka huu kuanza kupatikana rasmi katika Smart TV ambazo zinatumia mfumo wa webOS 5.0 na webOS 6.0 ambapo itarahisisha kuangalia video fupi za TikTok katika TV.

Picha ya Mtandao wa TikTok

Kukuwa kwa Teknolojia kumeufanya mtandao huu kuchukua soko la Smart TV, kwa kutoa Application kwa watumiaji wa Android TV na sasa imetanua wigo wake kwa watumiaji wa webOS ikiwa huu ni mpango mzuri kama ilivyo kwa Apple TV Plus, Netflix na YouTube walivyofanikiwa kuwa na Apps katika smart TV.