Jumanne , 9th Nov , 2021

Mshauri wa masuala ya uchumi na biashara, Dkt. Mowo Ringo, amesema kuwa watu wanatakiwa kutokufikiri kwamba kipimo pekee cha mafanikio ni kuwa na pesa, na kusema kwamba pesa ni muhimu lakini kuna sehemu pesa hushindwa kukwamua jambo mfano kuokoa uhai au kuepusha ugonjwa fulani.

Mshauri wa masuala ya uchumi na biashara, Dkt. Mowo Ringo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 9, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, na kusema kwamba mafanikio hupimwa kulingana na malengo ambayo mtu amejiwekea.

"Watu wasichanganye wakafikiri mafanikio ni pesa, maisha sio pesa tu, kuna sehemu nyingine pesa haiwezi kufungua, tunaweza kusema pesa si kila kitu lakini ina nguvu ya kukusogeza kwenye mambo mengi sana,watu watafute pesa ila wasiichukulie kama ni solution kwa kila kitu," amesema Dkt. Ringo.