Jumamosi , 16th Jul , 2022

Hakuna kiasi cha pombe kinachofaa kwa watu chini ya umri wa miaka 40, hasa kutokana na vifo vinavyotokana na pombe kwa watu chini ya umri huo kwa mujibu wa utafiti mpya wa Chuo Cha Dawa cha Washington.

Kiasi kidogo cha pombe kinaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa, kiharusi na kisukari.

Utafiti huo uliofanywa kwa watu kuanzia umri wa miaka 15 hadi 95 katika mataifa 204 duniani, uligundua kwamba unywaji pombe hauna faida yoyote kiafya kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40 lakini una athari kubwa kama vile ajali za magari na vifo.

Athari ni ndogo kwa watu wenye umri kuanzia miaka 65 ambao wengi huzingatia hunywaji wa pombe kwa kiwango kutokana na matatizo ya kiafya.