Paul Makonda atangaza kupata watoto mapacha

Jumatatu , 31st Aug , 2020

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram anaoumiliki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, amehabarisha kupata watoto mapacha ambao ni wa jinsia ya kiume na ya kike.

Kwenye picha ni Paul Makonda na mke wake

Paul Makonda amesema pamoja na magumu anayopitia lakini anamshukuru Mungu kwa nuru ambayo anamuangazia na kwa nyakati zote ambazo yupo naye.

"Heshima na mamlaka zako Mungu wa mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwa kuwa hujawahi kuniacha hata dakika moja, pamoja na mapito,magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya roho mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali taa iwakayo ndani yako ikazimika

"Mimi niliyeitwa tasa ulinipa mtoto Keagan ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake, ukaona haitoshi leo umenipa Double Portion, leo Mungu wangu umenipa Mapacha tena wa kiume  na wakike, hii yote ni kutangaza ukuu wako maishani mwangu" ameongeza