Jumanne , 12th Jul , 2022

Mwanafunzi wa chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Lindi, Melkczedeck Bruno alifika katika ofisi za East Africa TV na East Africa Radio siku ya leo na kukabidhi mchango wa taulo za kike pakiti 68 kupitia kampeni ya Namthamini ambazo zitaweza kusaid watoto wa kike 6 shuleni kwa mwaka mzima

Mkuu wa Idara ya Michezo East Africa TV na East Africa Radio, David Kampista (kushoto) akipokea mchango wa taulo za kike kutoka kwa Melkczedeck Bruno.

Bruno anasema wakati kampeni hii inaanza mwaka 2017 alikuwa bado kijana mdogo, alitamani kushiriki kuchangia lakini hakuweza. Mwaka huu alijipanga na ametimza ahadi yake ya kusaidia wanafunzi wa kike mashuleni.

Kwa pamoja tunaweza kutokomeza sifuri kwa watoto wa kike mashuleni  kwa kutengeneza mikakati dhidi yao na kuwapa elimu ya kutosha.