Jumatatu , 23rd Oct , 2023

Siku 11,478 kwenye uso wa Dunia hazikutosha kwa wale walio mpenda; Bobi anashikilia rekodi ya kuwa mbwa mzee kuwahi kuishi na amefariki akiwa na jumla ya miaka 31 na siku 165.

 

Ameshikiria rekodi hiyo ya kutambulika kama mbwa mzee zaidi kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia, Mwezi wa pili mwaka huu.

Kwenye makala iliyoandaliwa na Ted Kerasote, inaelezea maisha ya Bobi kama mbwa ambaye alifanikiwa kuishi maisha marefu kwa sababu alikula vizuri ikiwemo nyama na mboga mboga kwa wingi na samaki pia, Bobi alizingatiwa upande wa chanjo kwenye kila wakati ambao alihitajika kuchoma chanjo.

Bobi kwenye maisha yake inatajwa hakuwa hakipata nafasi ya kuchangamana na mbwa wengine wa mtaani hivyo badala yake alikuwa anatumia muda mwingi na familia iliyomtunza hali iliyomfanya kuwa na uangalizi mzuri zaidi.