Mazoezi dawa ya magonjwa yasiyoambukiza

Jumamosi , 29th Aug , 2020

Ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha udhoofu katika mwili na kupelekea kifo, wananchi wametakiwa kujiwekea tamaduni za kufanya mazoezi mara kwa mara.

Mazoezi

Akizungumza na EATV mkufunzi wa masuala ya afya na lishe bora Godrick Charles, amesema kuwa suala la afya limekuwa halizingatiwi kama tamaduni mpaka pale utakapotolewa ushauri kutoka kwa Daktari pekee hivyo kutaka jamii kubadilika 

"Ukweli tafiti nyingi zinaonesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamesababishwa na mitindo ya maisha namna ya kula, kunywa na mengine ni muhimu sana yakazingatiwa ili kuepusha athari za kiafya zaidi", amesema Charles.

Kwa upande wao washiriki wa mazoezi hayo ambao wengi wao ni wafanyakazi wa taasisi na kampuni mbalimbali, wamesema kuwa muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika shughuli za uzalishaji na kusahau mambo muhimu ya kuzingatia katika kulinda afya zao, huku akisisitiza umuhimu wa kutenga muda wa kufanya mazoezi na kuwaona wataalamu wa afya kwa ajili ya ushauri ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.