Mambo 5 ya kufanya kwa mtu aliyeungua moto

Jumanne , 14th Jul , 2020

Mara nyingi katika matukio ya ajali huwa kunakuwa na uhitaji mkubwa wa huduma ili kuepusha kutokea kwa madhara zaidi pamoja na kuepusha vifo.

Jeraha la moto

Moja ya matukio hayo ya ajali ni pamoja na moto ambao huwa unapelekea watu kuungua. Kupitia kipindi cha Dadaz cha EATV, Dr. Meshack Kinyuli ametoa elimu kuhusiana na mambo muhimu ya kufanya kwa mtu aliyeungua kwa moto.

Dr. Kinyuli ameanza kwa kufafanua nini maana ya jeraha la moto ambapo amesema jeraha la moto ni pale ambapo mwili hasa eneo la ngozi linakuwa na joto kuzidi kawaida, na kuyagawa majeraha ya moto kutokana na kuungua, kuunguzwa na maji au kemikali, umeme na mvuke.

"Mambo ya kuyazingatia kwa mtu aliyepatwa na jeraha lolote la moto, kwanza ni kuondoa moto eneo la tukio, pili ni kuondoa mavazi yake na vitu vingine vilivyoushika mwili wake kama mkanda na nguo lakini kama vitu hivyo vimeshikana kabisa na mwili visitolewe bali asubiriwe daktari", amesema.

"Mengine ya kuzingatia ni kuhakikisha anapumua vizuri na siwekewe mto kichwani kwani itampa ugumu kupumua. Pia mtu anayeungua moto moja kwa moja hapaswi kukimbia bali agalegale kwenye mchanga na hii ni kwa moto wa kawaida pamoja na kufunika eneo athirika kwa kitambaa chenye ubaridi", ameongeza.

Tazama hapa amelezo yote kutoka kwa Dr. Kinyuli.