Jumatano , 18th Mei , 2022

Licha ya mtoto wake kuwa tajiri namba 1 Duniani, haimzuii Maye Musk mama mzazi wa Elon Musk kuendelea na kazi ya mitindo akiwa na umri wa miaka 74.

Maye Musk katika jarida la 'Sports Illustrated Swimsuit'

Maye Musk amekuwa mwanamitindo mzee kuwahi kutokea katika jarida la 'Sports Illustrated Swimsuit' akichuana na Kim Kardashian na Ciara ambao pia wametokea katika jarida hilo kwa mwaka 2022.

Maye amefanya kazi hiyo kwa miaka 50 na hata kabla ya kumzaa Elon Musk, na alishawahi kutokea katika majarida makubwa kama Vogue.