Mama auza gari yake kisa kununua maua

Jumanne , 24th Nov , 2020

Kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV mshauri wa utunzaji maua na bustani Hawa Mniga amesema anapenda sana maua hali iliyopelekea hadi kuuza gari yake aina ya Spacio kwa milioni 5 ili kununua maua aweke nyumbani kwake.

Picha kubwa ni bustani ya maua, picha ndogo ni gari aina ya Spacio

"Tangu mdogo nilikuwa napenda maua, nilikuwa na gari yangu ya Spacio nikaiuza kwa milioni 5 ila pesa yote nikaaingiza kwenye garden, hicho kitu ndiyo kikanituliza nyumbani na nitayapanda mpaka nizeeke" amesema Hawa Mniga 

Aidha akaendelea kusema "Mimi siuzi maua ila napenda kuona nyumba yangu ikiwa hivyo, uzuri wake yanazaa unaweza ukanunua ua moja kwa shilingi elfu sabini ila baada ya miezi kama saba linatoa watoto, kwa hiyo wale watoto utawauza kutokana na size kuna ya elfu 30 au elfu 25".

Show hiyo ya DADAZ huruka hewani kupitia East Africa TV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 5:00 Asubuhi hadi 6:00 Mchana ambapo huwa kuna wageni mbalimbali kama watu wa taaluma, lifestyle, familia, mahusiano na burudani.