Alhamisi , 12th Oct , 2023

Ikiwa kama wewe ni mwanafunzi wa elimu ya juu na unahitajika kuwa na ''calcutaor'' zaidi ya moja kwa ajili kukusaidia kwenye shughuli zako za ki-elimu nasi SUPATECH tunaileta hii kwako.

 

Kabla ya kuendelea labda tuweke sawa kwanza hapa, tunaposema ''calculator'' zaidi ya moja ni kwa maana hautakuwa na haja ya kununua ''calculator'' zaidi ya moja kwa ajili ya kazi tofauti tofauti mfano Basic Scientific calculators, Graphing calculators, Financial calculators na aina nyingine za calculator

Kuna aina tofauti tofauti za ''calculator'' ipo aina moja ya kwanza ambayo wengi ndiyo tunaitumia inafahamika kama ''Basic calculator'' ambayo hufanya kazi ndogondogo kama vile hesabu za kujimlisha, kutoa, kugawanya na hesabu nyingine za kawaida

Aina nyinginezo za calculators zimegawanyika kutokana na somo au unaweza kusema kazi husika ni kama vile ''Scientific calculators, Graphing calculators, Financial calculators na aina  nyinginezo.

Msingi wa yote hayo ni kukufahamisha kuhusiana na hii wavuti ambayo imesheheni zaidi ya calculator ''3517'' ndani yake na ni bure kuitumia, hii inaitwa ''omnicalculator.com'' itakurahisishia sana kwenye kukokotoa kazi mbali mbali.

Picha: GeeksforGeeks