Jumatano , 30th Mar , 2022

Kundi la Taliban limeagiza wafanyikazi wote wa serikali nchini Afghanistan kuwa na ndevu na kuzingatia kanuni za mavazi au kufukuzwa kazi kama wakishindwa kufanya hivyo.

Picha ya baadhi ya wanaume wenye ndevu Afghanistan

Taarifa hiyo inasema wawakilishi kutoka Wizara ya Uenezi wa Utu wema wamefanya doria kwenye ofisi za serikali Jumatatu ili kuangalia kama watumishi wanafuata sheria mpya.

Wafanyakazi walikuwa wakielekezwa kutonyoa ndevu zao na kuvaa mavazi yenye urefu, suruali iliyolegea na kofia au kilemba.

Pia wameambiwa hawataweza kuingia ofisini bila ndevu na kutishiwa kupoteza kazi zao iwapo hawatafuata kanuni za mavazi zilizowekwa na utawala wa Kiislamu wenye msimamo mkali.