Ijumaa , 6th Oct , 2023

Kama umekuwa sehemu ya wachache ambao wamekumbana na changamoto hii ya simu kukatika yenyewe wakati unajaribu kuwasiliana na mtu basi hizi ni baadhi ya njia ambazo unaweza kuzitumia kutatua changamoto hiyo.

 

Niweke sawa hapa kwanza hii ni kwa wale ambao wame-update IOS iwe ya 16 au 17 alafu ndiyo wakakumbana na changamoto hii kwa mara ya kwanza.

Njia ya kwanza (1). Ingia kwenye Setting - Mobile service - Network selection - ukikuta iko ''automatic'' sogeza ijizime alafu chagua jina la mtandao husika unaotumia kwenye simu yako - washa Airplane mode kwa sekunde 20 - Restart simu yako.

Njia ya Pili (2). Ondoa laini yako ya simu alafu iweke tena kwenye simu yako

Njia ya Tatu (3). Ingia kwenye setting - Mobile service - Wi-Fi calling - ukikuta imezimwa iwashe - rudi kwenye mobile data option ichague - nenda kwenye voice and data - alafu kama ilikuwa 4G basi chagua 3G 

Njia ya Nne (4). Ingia setting - chagua General - ingia kwenye Transfer or Resert iphone - chagua Resert - Resert network setting (lakini chaguo hili litaondoa baadhi password za Wi-Fi ambazo ulikuwa ume-save kwenye simu yako) 

Hizi ni njia ambazo unaweza kuzitumia, ikiwa moja kati ya njia hizi hazijafanya kazi kwenye simu yako basi ni vyema ukapata msaada kwa fundi wa simu unayemuamini.