Hedhi App yazinduliwa kusaidia Afya ya uzazi

Jumatano , 21st Oct , 2020

Kampuni ya Anuflo Industries Limited imezindua ‘App’ ambayo itawawezesha wanawake na wasichana nchini kuwasiliana na madaktari kupitia simu zao bila kuonana na kutatua changamoto za afya ya hedhi pamoja na elimu ya masuala mazima ya afya ya uzazi.

Mkurugenzi Kampuni ya Anuflo Industries Limited, Flora Njelekela.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Anuflo Flora Njelekela amesema kuwa App hiyo itasaidia kurahisha huduma kwa wakina mama wengi kupitia madaktari bingwa watakaokuwa wakiwahudumia.

Kuna wanawake wanapitia changamoto kadhaa ikiwemo kukosa hedhi au kupata matatizo wakati wa hedhi, lakini wanashindwa kuongea mbele ya madaktari kwa hiyo kupitia App hii wataweza kuwasiliana na madaktari na kupatiwa maelekezo na kusaidiwa matatizo yao”, amesema Flora.

Mmoja kati ya madaktari watakaotoa huduma hizo kwa watakaojitokeza kupakua application hiyo, Dkt. Berno Mwambe amesema kuwa mawasiliano baina ya mteja na daktari ni siri yao wawili.