Jumanne , 3rd Oct , 2023

Kwenye moja ya maboresho ya kushangaza ambayo yamefanywa na kampuni ya Apple Inc mwaka huu ni kubadilisha mfumo wa chaji kwenye simu zao, kutoka kutumia ''Lightning cable" mapaka kutumia ''USB C'' wenyewe tunaifahamu kama ''Type-C''

 

Sasa ikiwa kama hii ya kubadilishwa kwa mfumo wa kuchaji kwenye toleo jipya la iPhone ''iPhone 15" itakuwa imekushangaza, basi tambua fika onyo limetolewa kwa wamilikiwa simu hizo.

 Kwa mujibu wa wavuti wa ''CNMO'' umetoa taarifa ilioyoko kwenye mfumo wa ripoti ukitoa onyo kwa watumiaji wa simu toleo jipya la iPhone kuepuka kutumia chaja za ''Android'' kwani zitapelekea simu hizo kuungua.

Mfumo wa USB-C umezoeleka kwa muda mrefu hivi sasa kwa watumiaji wa simu za Android, lakini ni mpya wa watumiaji wa iPhone hivyo kuwafanya baadhi ya watumiaji wa simu toleo hili jipya kutumia chaji za Android.