Jumatano , 18th Mei , 2022

Katika mji wa Izmit, Uturuki mwanaume aliyetambulika kwa jina la Furkan Ciftci alifariki baada ya kuzama baharini akijabu pozi la kwenye filamu ya Titanic kwenye meli akiwa na mpenzi wake Mine Dinar.

Mine Dinar (kushoto) na Furkan Ciftci

Wote wawili wana umri wa miaka 23, inadaiwa walikuwa wametumia kilevi kabla ya tukio hilo kutokea siku ya jumapili.

Furkan na Mine waliteleza wakati wanajaribu kukaa katika pozi hilo na kuangukia baharini, Mine aliwahi kuokolewa ila Furkan alizama ndani ya maji na mwili wake ulipatikana baada ya masaa mawili.