Alhamisi , 17th Mar , 2022

Mrembo Tara Jayne McConachy aka "Plastic Surgery Queen'' au ''Human Barbie Doll'' kutokea nchini Australia mpaka sasa ametumia $200,000 sawa na Tsh million 463 ili kupata muonekano alionao sasa.

Kabla na baada ya kufanya surgery.

Tara kwa sasa ana umri wa miaka 33, jana alifanya matembezi katika mji wa Melbourne akiwa na mama yake ili kuonyesha muonekano wake mpya wa ndoto zake baada ya kufanya surgery 5 za matiti, 6 za pua na mdomo, sura na makalio, na bado ana mapango wa kuendelea kufanya surgery kupendezesha mwili wake.

Alipata umaarufu baada ya kuonekana katika kipindi cha TV cha "Botched'' cha channel E! na mpaka sasa ana wafuasi zaidi ya 149,000 katika ukurasa wake wa instagram.