Jumamosi , 30th Oct , 2021

Mwanaume mmoja nchini Nigeria aitwaye Akintunde Adegbesan, amemfungulia mashtaka mwanaume aitwaye Sikiru Jamiu akimtuhumu kumuita 'Babe' mke wake alipomtumia ujumbe wa kumsalimia na kuandika 'Good morning babe' kupitia WhatsApp.

WhatsApp

Jamiu anakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika ndoa kati ya mwanaume huyo na mke wake aitwaye Opeyemi Adegbesan.

Kwa mujibu wa karatasi ya mashtaka iliyopo kwenye mitandao ya kijamii imeeleza kwamba Jamiu alimtumia ujumbe huo mke wa Adegbesan Septemba 19, 2021, majira ya saa 2:00 asubuhi.