Alhamisi , 25th Nov , 2021

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Evie Toombess (20) amefungua kesi dhidi ya Daktari aliyemsaidia mama yake kujifungua kwa madai ya kwamba yeye hakustahili kuzaliwa.

Picha ya Evie Toombess

Evie alizaliwa na tatizo la 'Spina Bifida' ambalo husababishwa na kutokukua vizuri kwa uti wa mgongo wa mtoto akiwa tumboni, pamoja na kuzaliwa na tatizo hilo Evie ni maarufu katika mchezo wa kuruka na farasi nchini Uingereza.

Evie anasema kama Dkt Phillip Mitchell angemshauri mama yake kutumia virutubisho vya 'Folic Acid' basi mama yake asingebeba ujauzito na yeye asingezaliwa na tatizo la 'Spina Bifida' ambalo humfanya kuvaa mirija masaa 24.