Jumatatu , 25th Oct , 2021

Mwanamke raia wa Mali, Halima Cisse,(26) ambaye mwezi Mei alijifungua watoto tisa kwa mkupuo mmoja ameonesha sura za watoto wake hao ambao watano ni wa kike na wanne wa kiume.

Watoto pacha wa Halima Cisse

Mwanamke huyo alijifungua katika kliniki ya Ain Borja Mjini Casablanca, Morocco, ambapo watoto wake hao waliwekwa kwenye mashine maalumu ya uangalizi hadi mwezi Agosti walipotolewa.

Halima na mume wake Kader Arby, (35) wamesema japo ni furaha kuwana watoto lakini bado wanawaza namna ambavyo wataweza kujiopanga kimaisha ili kuweza kuwalea pacha hao tisa na mwenzao mmoja ambao ni jumla ya watoto 10, licha ya serikali ya Mali kuwasaidia kulipa gharama za hospitalini.

Watoto hao pacha walizaliwa na uzito tofauti tofauti ambapo wengine walikuwa na kilogramu 0.5 na wengine kuwa na kilogramu moja na walizaliwa kwa msaada wa uangalizi wa madaktari 30.

Inadaiwa kuwa Halima Cisse amevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Nadya Suleman ambaye alizaa watoto wanane mwaka 2009.