Afunga TV kwenye Bodaboda ili kuvutia wateja 

Jumatano , 18th Nov , 2020

Dereva Bodaboda Shomari Ramadhan kutoka Mwenge Jijini Dar Es Salaam, ameamua kufanya ubunifu wa kuweka runinga (Television) kwenye pikipiki yake ili kuvutia zaidi abiria anaowapeleka safari kutumia usafiri wake.

Hii ndiyo Bodaboda yenye TV

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, dereva huyo amesema amefanya kazi hiyo ya bodaboda kwa miaka miwili na TV hiyo ameinunua miezi miwili iliyopita kwa shilingi 130,000 na sasa hivi imeweza kumpatia faida kubwa.

"Nimeamua kufanya ubunifu huu wa kuweka TV ili kuwavutia abiria, muda mwingine nikikaa kijiweni kama nikikosa abiria huwa natulia kuangalia, abiria wengi kwanza huanza kwa kushangaa pili kupenda na kufurahi kwa kusema hawajawahi kuona pikipiki yenye TV pia huniuliza maswali mengi" ameeleza Shomari Ramadhan

Aidha ameendelea kusema TV hiyo inafanya kazi kwa kutumia 'system' za betri la pikipiki wala hajaongezea vitu vingi, na madereva wengi wa bodaboda wanatamani kuwa kama yeye ili kushawishi abiria zaidi.

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.