Alhamisi , 24th Sep , 2020

Kufuatia kuvuja kwa video zisizo na maadili mitandaoni zikimuonyesha  mwanafunzi anayedaiwa kusoma chuo cha usimamizi wa fedha, Wakili Getrude Diabene amesema kisheria ni kosa kujirekodi picha au video za utupu kabla hata kusambazwa.

Alama inayoonyesha hali ya tahadhari

Wakili Getrude Diabene amesema ikitokea picha au video kusambaa mitandaoni huwa wanaangalia imetokea kwenye mazingira gani, kisha wanaenda kwenye kanuni ambazo zinasema mtu huyo alikuwa na nia gani ya kusambaza,  kama alikuwa ana nia ya kumdhalilisha mwenziye  inakuwa kosa kisheria.

"Ukija kwenye sheria ya makosa ya mitandaoni kifungu cha 14 kinasema ni kosa kusambaza video au picha zenye kuashiria ngono, tena  wote wawili mnakuwa mmefanya kosa, adhabu yake ni miaka zaidi ya 10 jela, faini ya milioni 30 au vyote kwa pamoja, aliyesambaza atakuwa na kosa la jinai" amesema Wakili Getrude Diabene

Aidha Wakili huyo ameongeza kusema kwenye tukio kama hilo huwa kuna mambo mawili ambayo yanatokea kwa sababu kuna wale wanaotaka kurekodi wenyewe, pili kuna kurekodiwa bila ya kujua au kutekwa na kuleweshwa halafu unarekodiwa.