Jumatano , 7th Feb , 2018

Mfanyabiashara na mchekeshaji maarufu bongo Idriss Sultani amekiri wazi kwa sasa wanawake wengi na warembo wanamuogopa kuwa naye kwenye mahusiano kutokana na kazi yake pamoja na umaarufu alionao.

Idris amefunguka hayo leo akiwa kwenye kipindi cha Kikaangoni Live kinachorushwa kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV nakusema kwamba wanawake wanaoonekana sahihi kwake yaani wenye msimamo, akili na wasio tegemezi wanaogopa kuwa naye kwa  kudhani kwamba  maisha yao yatakuwa yakufatwa fatwa na mapaparazi pamoja na magazeti ya udaku.

Idris ameongeza kuwa wakati mwingine anadhani kazi yake ya uchekeshaji nayo pia ndiyo sababu pia akose wanawake wenye vigezo vyake kwani watu wanahisi kuwa anakuwa hayupo 'serious' katika suala zima la mahusiano.

"Kabla mtu hajakutana na wewe anakuwa ameshakujaji kila kitu kiasi kwamba mpaka anakufikia anaweza kusema huyu dogo kichaa. Wanahisi sisi 'comedian' hatupo serious hawadhani kama tunaweza kupenda lakini cha ajabu wenzetu huko nje ya nchi wanapata wanawake wazuri yaani pisiii kweli kweli.." Idris

Idriss ameongeza kwamba "kuwa mchekeshaji n moja ya kigezo kinachonifanya nisipate 'a proper women' ninayemtaka.

 

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.